Lukula ataja siri ya ushindi dhidi ya Fountain Gate

Kocha Mkuu Charles Lukula, amesema mabadiliko aliyofanya ya wachezaji wawili yaliifanya timu kuongeza kasi iliyotufanya kutoka nyuma na kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fountain Gate.

Lukula amesema ilibidi amtoe Daniela Mgoyi mapema kipindi cha kwanza na kumuingiza Esther Mayala ambaye aliituliza safu ya ulinzi kabla ya kufanya hivyo kwa Diana Mnali cha pili na kumuingiza Aisha Juma na kuifanya timu kuwa na uwiano mzuri wa kuzuia na kushambulia.

Lukula amewasifu wachezaji kwa utulivu waliokuwa nao ambapo licha ya kuwa nyuma kwa bao moja hawakutetereka na kupambana mpaka kufanikiwa kupata pointi tatu.

“Mchezo ulikuwa mgumu Fountain ni timu nzuri na imejipanga vizuri, nawapongeza wachezaji wangu kwa kazi kubwa waliyofanya na kusaidia kupatikana kwa alama tatu.

“Ligi ya msimu huu ni ngumu kila timu imejipanga, mchezo dhidi ya Fountain imeisha tunajipanga kwa mechi ijayo,” amesema Lukula.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER