Lukula afunguka siri ya ushindi

Kocha Mkuu Charles Lukula, amesema kilichofanikisha ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Determine Girls ni kuwajenga kisaikolojia baada ya kucheza kwa presha kipindi cha kwanza.

Lukula amesema kipindi cha kwanza tulipoteza nafasi nyingi ambazo ziliwafanya kucheza kwa presha na kufanya makosa kadhaa.

Lukula ameongeza kuwa baada ya kwenda mapumziko alizungumza na wachezaji na kuwaambia watulie na kucheza kawaida na hicho ndicho kilichosababisha tupate ushindi.

“Ni furaha kwangu kupata ushindi wa kwanza kwenye michuano mikubwa hii, tulicheza vizuri lakini tulipoteza nafasi nyingi kipindi cha kwanza na kutufanya kucheza kwa presha,” amesema Lukula.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER