Licha ya kutolewa Shirikisho Pablo awamwagia sifa wachezaji

Kocha Mkuu Pablo Franco, amewasifu wachezaji kwa kujituma muda wote wa mchezo ingawa tumetolewa Kombe la Shirikisho Afrika na Orlando Pirates kwa mikwaju ya penati 4-3.

Pablo amesema amefurahishwa na jinsi wachezaji walivyojituma na kujitahidi kufuata maelekezo kitu ambacho amejivunia.

Pablo ameongeza kuwa tutaendelea kusubiri kwa mwaka mmoja mwingine kufika nusu fainali ya michuano hii baada ya kupita miaka 29 ingawa amesema kiwango cha soka kimepanda ukanda wa Afrika Mashariki.

“Nawapongeza sana wachezaji wangu kwa moyo wa kujitolea kwa ajili ya timu licha ya kucheza pungufu uwanjani muda mrefu. Ulikuwa mgumu wakuvutia lakini tutasubiri kwa mwaka mmoja kufikia malengo yetu.

“Siku zote penati hazina mwenyewe ila nilichopenda ni jinsi wachezaji wangu walivyopambana. Pia niwapongeze Orlando walikuwa bora ndani ya dakika 90 sisi safari yetu imeishia hapa tutajipanga mwakani,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER