Licha ya kushinda kocha Simba Queens hajaridishwa na kiwango

Kocha Mkuu wa Timu yetu ya Wanawake ya Simba Queens, Hababuu Ally hajaridhishwa na kiwango cha nyota wake licha ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya PVP FC.

Kocha Hababuu amesema timu haijacheza vizuri kama alivyotarajia ingawa imeibuka na ushindi huo mnono.

Hababuu ameongeza kuwa kuelekea mchezo wa pili dhidi ya Lady Doves atayafanyia marekebisho mapungufu yaliyojitokeza ili kuhakikisha tunafanya vizuri.

Kocha Hababuu ameenda mbali zaidi kuwa tunahitaji kupata ushindi kwenye mchezo unaofuata ili kutinga nusu fainali.

“Hatukucheza vizuri mechi ya leo lakini tumepata ushindi mnono, tutajitahidi kuyafanyia marekebisho mapungufu yaliyojitokeza kabla ya mchezo ujao wa Jumanne dhidi ya Lady Doves,” amesema Kocha Hababuu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER