Leo tupo Benjamin Mkapa kuikabili Azam

Kikosi chetu leo kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC utakoanza saa 12:15 jioni.

Ni mchezo muhimu wa kupata alama tatu kwakuwa tunahitaji kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kumaliza katika nafasi mbili za juu.

Utakuwa mchezo mgumu kutoka nafasi tuliopo sisi pamoja na wapinzani wetu lakini tupo tayari kwa mapambano.

Mgunda afunguka…..

Kocha Mkuu Juma Mgunda amesema maandalizi ya mchezo yamekamilika na wachezaji wapo kwenye hali nzuri.

Mgunda amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri huku akikiri utakuwa mchezo mgumu kutokana na ubora wa Azam lakini tupo tayari kuwakabili.

Mgunda ameongeza kuwa Azam ni timu bora na ndio maana ipo nafasi ya pili kwenye msimamo lakini tumejipanga kuhakikisha tunashindana na kushinda.

“Itakuwa mechi nzuri, Azam ni timu bora lakini tumejipanga kucheza na timu bora na tupo tayari kupambana ili kupata ushindi,” amesema Mgunda.

Kazi ongea kwa niaba ya wachezaji……

Mlinzi wa kati, Hussein Kazi amesema wachezaji wapo tayari kupigania timu ili kupata pointi tatu muhimu.

“Kwa upande wetu wachezaji tupo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho, tunajua itakuwa mechi ngumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda,” amesema Kazi.

Tulitoka sare mechi ya mwisho…

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi uliopigwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Februari 9 mwaka huu tulitoka sare ya kufungana bao moja.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER