Leo Tunacheza Fainali dhidi ya Jwaneng

Saa moja usiku tutashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Jwaneng Galaxy katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo huu ni fainali kwetu au tunaweza kuuita kufa au kupona. Tunahitaji kushinda mechi ya leo ili kujihakikishia nafasi ya kutinga robo fainali.

Ni ndoto ya kila Mwanasimba kuiona timu yake ikitinga robo fainali leo. Hakuna sababu yoyote ambayo itaeleweka kama matokeo yatakuwa hatofauti.

Katika michezo wa leo hatuangalii matokeo ya timu nyingine ili kujihakikishia kufuzu. Tukishinda mechi yetu tutafikisha pointi tisa ambazo Wydad Casablanca ambao wanatufuatia wanaweza kuzifikia lakini bado tutakuwa na faida ya bao moja tuliopata tulipokutana.

Benchikha atoa kauli……

Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha amesema tunahitaji kushinda kwa ajili ya mashabiki wetu ambao wamekuwa nasi katika kipindi chote na wanastahili kupata furaha kwenye mchezo wa leo.

“Sisi tunatakiwa kushinda hatumuangalii mtu wala matokeo ya timu nyingine, hii ndio faida yetu, tunatakiwa kuwa imara tushinde kwa ajili ya mashabiki wetu na Watanzania wote wanaotusapoti,” amesema Benchikha.

Ni Mechi ya Kisasi…..

Oktoba 24, 2021 tulikutana na Jwaneng Galaxy katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na walitufunga mabao 3-1 na kututoa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa.

Ndio maana tunaita kisasi kwakuwa tunakumbuka mara ya mwisho walituachia huzuni na leo wamekuja tunataka kulipa kisasi na kutinga robo fainali.

Ahmed Ally awaita mashabiki kwa Mkapa….

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu Ahmed Ally amesema maandalizi ya mchezo yamekamilika na kila kitu kipo kwenye mstari kilichobaki ni mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani ili tupate tiketi ya kufuzu robo fainali.

“Kama hamasa zimefanyika za kutosha na timu imepata maandalizi mazuri kilichobaki ni mashabiki kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu na lengo letu ni kuingia robo fainali,” amesema Ahmed.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER