Leo tunaanza safari ya NBCPL 2023/24

Kikosi chetu leo kinaanza kampeni ya kuhakikisha tunapambana kwa kila hali kupata alama tatu katika Uwanja wa Manungu Complex.

Leo tutakuwa wageni wa ‘Wakata Miwa’ Mtibwa Sugar katika mchezo huo ambao utaanza saa 10 jioni.

Tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Mtibwa hasa tukiwa tunafahamu tupo ugenini.

Robertinho aahidi soka safi…….

Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema tunahitaji kucheza soka safi pamoja na kupata matokeo chanya ya ushindi.

Robertinho amesema Simba ni timu kubwa Afrika na hilo linapaswa kuonekana uwanjani kwa kutandaza soka safi.

“Tunahitaji kucheza soka safi na kushinda, hilo ndilo lengo letu. Simba ni timu kubwa na ipo juu kwenye viwango vya ubora wa Afrika, wapinzani wetu wanapaswa kutuheshimu nasi tunawaheshimu pia,” amesema Robertinho.

Kwa upande wake mlinzi wa kulia, Israel Patrick amesema utakuwa mchezo mgumu kutokana na ubora wa Mtibwa lakini tupo tayari kupambana huku akiwaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani.

“Tunajua mchezo utakuwa mgumu, Mtibwa ni timu nzuri lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda. Tunaomba mashabiki wetu mje kwa wingi uwanjani kutupa sapoti,” amesema Israel.

Manula, Inonga kuikosa Mtibwa…….

Katika mchezo wa leo tutakosa huduma ya wachezaji wetu wawili ambao ni majeruhi.

Mlinda mlango Aishi Manula na mlinzi wa kati Henock Inonga aliyeumia bega katika mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii hawatakuwa sehemu ya mchezo wa leo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER