Lakred aanza mazoezi rasmi

Mlinda mlango mpya, Ayoub Lakred (28) raia wa Morocco amejiunga na kikosi na leo ameanza rasmi mazoezi pamoja na wenzake.

Lakred tumemsajili wiki iliyopita kutoka kwa Mabingwa wa Morocco, FAR Rabat tayari amejiunga na kikosi na yupo mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa keshokutwa Alhamisi.

Lakred amefanya mazoezi moja kwa moja na walinda milango wenzake Ally Salim, Hussein Abeli na Ahmed Feruz chini ya kocha Daniel Cadena.

Pamoja nakuwa ni siku yake ya kwanza mazoezini akiwa na kikosi chetu Lakred ameonyesha uwezo mkubwa na kuyafuata vema maelekezo aliyokuwa akipewa na kocha Cadena.

Tunaamini uwezo wa Lakred utazidi kuimarisha kikosi chetu na kocha mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ atakuwa na wigo mpana wa uchaguzi wa timu kulingana na mchezo husika.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER