Kwaheri Augustine Okrah

Uongozi wa klabu unatangaza rasmi kuachana na kiungo wetu mshambuliaji Augustine Okrah baada ya kumalizika Msimu wa mashindano wa 2022/23.

Okrah raia wa Ghana amemaliza mkataba wake ndani ya klabu na mchezaji huyo hatoongezewa mkataba mpya.

Okrah alijiunga nasi mwanzoni kwa msimu huu akitokea Benchem United ya nyumbani kwao Ghana ambapo ameonyesha uwezo mkubwa katika mechi zote alizocheza.

Katika msimu mmoja aliohudumu ndani ya kikosi chetu Okrah amekuwa na mchango mkubwa akicheza mechi 17 na kufunga mabao manne na kusaidia kupatikana kwa jingine moja.

Kuondoka kwa Okrah ni ishara ya kuanza rasmi utelekezaji wa maboresho ya kikosi chetu kuelekea msimu ujao wa mashindano.

Uongozi wa klabu umedhamiria kufanya maboresho makubwa kwenye kikosi kuanzia eneo la benchi la ufundi kwa kuongeza watalaamu zaidi pamoja na wachezaji wenye hadhi kubwa na ubora wa kuitumikia Simba.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER