Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa Nusu Fainali ya Michuano ya Azam Sports Federation Cup kati yetu na Yanga ambapo cha chini kitakuwa Sh 10,000.
Viingilio hivyo vimetangazwa leo ikiwa ni siku nne kabla ya mchezo wenyewe ili kuwapa nafasi mashabiki kukata tiketi mapema.
Mchezo na watani wa jadi huvuta hisia za mashabiki wengi ambapo wengine hutoka nje ya nchi kuja kushuhudia.
Hivi hapa viingilio vyenyewe
VIP A Sh 30,000
VIP B Sh 20,000
Mzunguko Sh 10,000