Kurejea majeruhi kutuongezea nguvu kikosini dhidi ya Berkane

Nahodha Msaidizi Mohamed Hussein (Zimbwe Jr) amesema kurejea kwa wachezaji waliokuwa majeruhi wameongeza nguvu kubwa kuelekea mchezo wetu wa Jumapili wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane kutoka Morocco.

Zimbwe Jr amesema unapojiandaa na mechi ngumu ya kimataifa inakuwa vizuri kuwa na kikosi kamili ambapo kocha anakuwa na wigo mpana wa kupanga timu.

Wachezaji ambao walikuwa na majeruhi na tayari wamerejea mazoezi ni Kibu Denis, Chris Mugalu, Sadio Kanoute, Jonas Mkude na Aishi Manula.

“Tunaenda kwenye mchezo mgumu, jambo la kushukuru tunaenda tukiwa na kikosi kamili wachezaji wenzetu waliokuwa majeruhi wamerejea na wameongeza nguvu kikosini,” amesema Zimbwe Jr.

Zimbwe ameongeza kuwa alama tatu za mchezo wa Jumapili zitaweka wazi mustakabali wetu kwenye kundi na kuongeza morali kuelekea mechi mbili zilizobaki.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER