Kocha wa zamani Real Madrid kumrithi Gomes

Klabu yetu imeingia mkataba wa miaka miwili na Kocha Pablo Franco (41) raia wa Hispania kukinoa kikosi chetu kuanzia sasa.

Pablo anachukua nafasi ya Didier Gomes raia wa Ufaransa ambaye mkataba wake ulisitishwa wiki mbili zilizopita baada ya makubaliano ya pande zote.

Kabla ya kujiunga nasi Pablo alikuwa anaifundisha Al Qadsia SC ya Quwait kuanzia 2019 hadi 2021.

Mwaka 2015 Pablo alikuwa Kocha Mkuu wa Getafe inayoshiriki Ligi Kuu nchini Hispania.

Pablo ambaye ni muumini wa soka la kushambulia alikuwa Kocha Msaidizi wa Real Madrid mwaka 2018 chini ya Kocha Julen Lopetegui na baadaye Santiago Solari.

Pamoja na kuwa muumini wa soka la kushambulia pia anamudu umiliki wa mpira kwa staili ya Hispania ya pasi nyingi ‘tik taka’ ambayo ndiyo falsafa ya Simba.

Kocha huyo mwenye Elimu ya UEFA Pro na elimu ya juu ya viungo na usomaji wa michezo, Simba inaamini ujio wake utaongeza ufanisi kwenye eneo lake la ufundi.

SHARE :
Facebook
Twitter

12 Responses

  1. Fanyeni usajili wa maana dirisha dogo
    Anzeni kumrudisha Okwi na Kahata
    Kisha dirisha kubwa chukueni Mukoko hapo kwa mazuzuu
    Kisha mkasake mshambuliaji wa maana
    Hawa kina Duncun Nyoni sijui kanoute watoeni kwa mkopoo hukoo

  2. Inabidi kuboresha upatikanaji wa haraka wa taarifa za klabu yetu maana mashabiki Huwa tuna hamu ya kupata taarifa Kwa haraka

  3. hbari mwanasimba napenda kupendekeza katika kikosi cha sima sc sio kwamba ni kibaya bali wachezaji wanakosa mbinu za kuweeza kufunga na munganiko wa baazi ya wachezaji wapya na waliopo bdo hauja kaa swa alafu kwa nni banda anakaa benchi na pia naimani na kocha aliyekuja atalifanyia kazi shida tulionayo asante

Leave a Reply to Ibrahim Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER