Kocha Lukula afunguka mipango yake dhidi ya Green Buffaloes

Kocha Mkuu Charles Lukula, amesema mchezo wa kesho dhidi ya Green Buffaloes kutoka Zambia ni kama fainali kwa kuwa tunahitaji ushindi ili tufuzu hatua ya nusu fainali.

Lukula amesema mchezo huo ambao utapigwa katika Mji wa Marrakech saa nne usiku kwa saa za nyumbani utakuwa mgumu kwa sababu kila timu inahitaji ushindi ili kufuzu na kikosi chetu kipo tayari kwa ajili ya mtanange huo.

Kuhusu hali ya wachezaji, Lukula amesema wapo vizuri na morali ipo juu kufuatia ushindi wa mabao 2-0 tuliopata juzi dhidi ya Determine Girls.

“Mchezo wa kesho ni muhimu kwetu na ni lazima tushinde ili tuingie hatua ya nusu fainali, tunajua utakuwa mgumu sababu wapinzani wetu pia wanaitaka nafasi hii. Tumejipanga na tupo tayari kwa mapambano,” amesema Lukula.

Kwa upande wake kiungo, Philomena Abakah amesema wachezaji wapo vizuri, wameandaliwa kimwili na kiakili tayari kwa mchezo huo wa kuamua hatma.

“Ni mchezo ambao tunapaswa kushinda ili kufuzu nusu fainali, itakuwa mechi ngumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda,” amesema Philomena.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER