KOCHA GOMEZ AKUNWA NA VIWANGO VYA NYOTA SIMBA

Kocha Mkuu, Didier Gomez Da Rosa amevutiwa na viwango vilivyoonyeshwa na wachezaji wetu vilivyozaa ushindi wa bao moja bila dhidi ya Al Ahly katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kocha Da Rosa amesema hawezi kumsifia mchezaji mmoja mmoja badala yake amekimwagia sifa kikosi kizima kwa kuonyesha kandanda safi muda wote wa mchezo.

“Siwezi kumsifia mchezaji mmoja kwenye ushindi wa leo, nawasifu wote kwa kupambana na kuonyesha soka safi,” amesema kocha Da Rosa.

Aidha, baada ya kupaa kileleni mwa msimamo, Kocha Da Rosa amesema ni jambo zuri ingawa bado amesisitiza kazi bado ni kubwa mbeleni.

“Kazi bado ni kubwa lakini kutokana na timu zote kwenye kundi letu kuwa bora, lakini tuna furaha kwa ushindi wa leo, tunaongoza kundi na tumepata ushindi kwenye mechi mbili mfululizo haikuwa kazi rahisi,” amesema Kocha Da Rosa.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER