Kocha Gomez afunguka sababu ya kutoa ‘dozi kubwa’ kwa Mtibwa

Kocha Mkuu, Didier Gomez ameweka wazi sababu ya ushindi wa mabao 5-0 tuliopata dhidi ya Mtibwa Sugar kuwa ni kucheza kwa nidhamu na kujituma.

Licha ya kufahamu Mtibwa haipo kwenye kiwango bora lakini Kocha Gomez aliwataka wachezaji kutowadharau na kucheza kwa nidhamu sababu tulihitaji kupata pointi tatu kwenye mchezo wa leo.

Gomez hakuacha kuwasifia wachezaji kwa kiwango safi walichoonyesha huku akisisitiza kuelekeza nguvu katika mechi tatu za Kanda ya Ziwa.

“Tunafurahi kupata alama tatu ambazo zimezidi kutusogeza kileleni, tulicheza kwa nidhamu na wachezaji walifuata maelekezo tuliyowapa,” amesema Kocha Gomez.

SHARE :
Facebook
Twitter

3 Responses

  1. Kwa Simba hii sioni haja ya kukaa na mawazo Kama huwezi kuwashinda basi ungana nao. Nahisi huu usemi wautumie vizuri timu pinzani Kama wanaona shida tunawakaribisha kikundi chao chote Cha uto.. wawe Mashabiki zetu😂🤣

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER