Kitta: Tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa maboresho ya katiba

Mwenyekiti wa Kamati ya Maboresho ya Katiba, Hussein Kitta amesema kazi waliyofanya ya kurekebisha katiba kwa mujibu wa maelekezo ya Serikali imefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Kitta amesema marekebisho yote waliyopendekeza yamepitishwa na wanachama isipokuwa kipengele kimoja cha uwakilishi wa mkutano mkuu ndicho kilichokataliwa na pia hakiwezi kukwamisha mchakato wa kuelekea mabadiliko ya undeshaji wa Klabu kwa mfumo wa hisa.

Kitta ameongeza kuwa Serikali iliiagiza kamati hiyo kufanya marekebisho ya sehemu sita kwenye katiba ambayo ni Uteuzi wa Bodi ya Wadhamini, Nafasi ya Mwenyekiti ilikuwa haitajwi kwa uwazi, Kutaja malengo ya klabu.

Mengine ni Utaratibu wa Uchaguzi Mkuu unaofaa kwa wanachama kuhudhuria, Kama kuna ulazima kuwa na chombo cha Simba Sports Club Holding Company ambayo inashika hisa na kifungu cha asilimia moja kushikwa na Mwenyekiti kwa niaba ya wanachama na vyote vimepitishwa.

“Ni jambo la kumshukuru Mungu tumefikia hatua nzuri marekebisho tuliyofanya yamepitishwa kwa asilimia kubwa ni kipengele kimoja tu cha uwakilishi wa Wanachama kwenye mkutano mkuu ndicho hakijapata lakini hakiwezi kukwamisha chochote kwenye mchakato wa uendeshaji wa klabu,” amesema Kitta.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER