Kitta aongezwa Bodi ya Wakurugenzi

Rais wa Heshima ambaye ni muwekezaji wa klabu, Mohamed Dewji ‘Mo’ amemteua Hussein Kitaa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu.

Kitta alikuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi miaka minne iliyopita upande wa wanachama baada ya kuchaguliwa kupitia uchaguzi mkuu.

Kitta anaungana na Wajumbe wengine wanne ambao wameteuliwa na Rais Mo miezi mitatu iliyopita wakiwa upande wa muwekezaji.

Wajumbe hao walioteuliwa na Rais Mo kabla ya Kitta ni Dk. Raphael Chageni, Hamza Johari, Zulfikar Chandoo na Rashidi Shangazi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER