Kipaumbele kuingia makundi, ushindi mnono baadaye

Kocha Msaidizi Thierry Hitimana, amesema katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy utakaopigwa Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa tunahitaji kupata ushindi ili kuingia hatua ya makundi.

Hitimana amesema kwenye mchezo huo tutaimarisha uchezaji wetu zaidi ya mechi ya kwanza ili kutoa burudani kwa mashabiki wetu lakini kuhusu idadi ya mabao hilo litafuata baadae kikubwa ni kupata ushindi na kusonga mbele.

“Tunachoangalia kwa sasa ni kupata nafasi ya kuingia hatua ya makundi, tumejipanga kuimarisha kiwango cha uchezaji wetu ili kutoa burudani kwa mashabiki.

“Tulitumia vizuri nafasi za mapema tulizopata katika mchezo wa kwanza, hizi ni dakika 90 nyingine mpya ambazo tutakuja na mipango tofauti ili kufanikisha kuingia hatua ya makundi,” amesema Hitimana.

Hitimana amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri morali ipo juu tayari kwa mchezo huo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER