Kinana Mgeni rasmi mchezo wetu dhidi ya Orlando

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Comrade Abdulrahman Kinana anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa mchezo wetu wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Orlando Pirates utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa leo saa moja usiku.

Kinana anakuwa miongoni mwa viongozi wa chama na serikali ambao wamewahi kualikwa kuwa wageni rasmi katika mechi zetu.

Mara zote tumekuwa tukialika viongozi wa serikali kwenye mechi zetu za kimataifa ili kuziongezea thamani.

Katika mchezo wetu wa mwisho wa hatua ya makundi uliofanyika Aprili 3 tulimualika Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER