Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya Raja Leo

Kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Mohamed wa Tano kuikabili Raja Casablanca saa saba usiku kwa saa za Tanzania katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amefanya mabadiliko ya wachezaji wawili ukilinganisha na kikosi kilichocheza na Horoya, Machi 18 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na kuibuka na ushindi mnono wa mabao 7-0.

Robertinho amemuanzisha beki Gadiel Michael kuchukua nafasi ya Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano na Erasto Nyoni aliyechukua nafasi ya Sadio Kanoute.

Kikosi kamili kilichopangwa:

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Gadiel Michael (2), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Erasto Nyoni (18), Clatous Chama (17), Mzamiru Yassin (19), Jean Baleke (4), Saido Ntibazonkiza (39), Kibu Denis (38).

 

Wachezaji wa Akiba:

Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5), Kennedy Juma (26), Nassor Kapama (35), Pape Sakho (10), John Bocco (22), Moses Phiri (25), Habibu Kyombo (32), Ally Salim (1).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER