Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya Prisons leo

Baada ya kukosekana katika mechi sita zilizopita zikiwamo tatu za mashindano na nyingine za kirafiki kutokana na majeruhi kiungo mkabaji Jonas Mkude leo ataanza katika mchezo wetu dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mkude atacheza sambamba na Mzamiru Yassin katika idara ya kiungo wa ulinzi huku Henock Inonga na Kennedy Juma wakisimama kama walinzi wa kati.

Habib Kyombo ataongoza mashambulizi pamoja na Moses Phiri huku Clatous Chama na Pape Sakho wakitokea pembeni kuwapa msaada.

Kikosi kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Kennedy Juma (26), Henock Inonga (29), Jonas Mkude (20), Clatous Chama (17), Mzamiru Yassin (19), Habib Kyombo (32), Moses Phiri (25), Pape Sakho (10).

Wachezaji wa akiba

Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5), Erasto Nyoni (18), Nassor Kapama (35), Augustine Okrah (27), Nelson Okwa (8), Dejan Georgijevic (7), Joash Onyango (16), Kibu Denis (38).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER