Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya Prisons leo

Kiungo mkabaji Taddeo Lwanga ataanza kwenye kikosi kilichopangwa kuikabili Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC utakaopigiwa Uwanja wa Sokoine saa 10 jioni.

Lwanga ametoka kupona majeraha wiki chache zilizopita ambapo mara kadhaa amekuwa akiingia kutokea benchi lakini leo ataongoza safu ya kiungo.

Lwanga atacheza sambamba na Erasto Nyoni katika idara hiyo huku mlinzi Joash Onyango akirejea kikosini baada ya mapumziko ya mechi tatu.

Medie Kagere ataendelea kuiongoza safu ya ushambuliaji akisaidiwa na viungo washambuliaji Peter Banda, Kibu Denis na Yusuf Mhilu.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Beno Kakolanya (30), Jimmyson Mwanuke (21), Gadiel Michael (2), Joash Onyango (16), Kennedy Juma (26), Taddeo Lwanga (4), Kibu Denis (38), Erasto Nyoni (18), Medie Kagere (14), Peter Banda (11), Yusuf Mhilu (27)

Wachezaji wa Akiba

Ally Salim (1), Henock Inonga (29), Jonas Mkude (20), Mzamiru Yassin (19), John Bocco (22), Hassan Mussa U20, Shafii Hassan U20, Kassim Omary U20.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER