Mshambuliaji Chris Mugalu na Bernard Morrison wamepangwa kuongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Orlando Pirates.
Mugalu na Morrison watapewa msaada wa karibu kutoka kwa mawinga wenye kasi, Pape Ousmane Sakho na Peter Banda.
Katika eneo la kiungo wa ulinzi Kocha Pablo Franco amewapanga Jonas Mkude na Taddeo Lwanga kutokana na Sadio Kanoute kuwa na kadi tatu za njano.
Henock Inonga leo atasimama na Pascal Wawa katika idara ya ulinzi wa kati wakati pembeni wakiwa kama kawaida Shomari Kapombe na Mohamed Hussein.
Kikosi Kamili kilivyopangwa
Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Henock Inonga (29), Pascal Wawa (6), Jonas Mkude (20), Pape Sakho (17), Taddeo Lwanga (4), Chris Mugalu (7), Bernard Morrison (3), Peter Banda (11).
Wachezaji wa Akiba
Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5), Erasto Nyoni (18), Kennedy Juma (26), Mzamiru Yassin (19), Kibu Denis (38), Rally Bwalya (8), Medie Kagere (14), Yusuf Mhilu (27).