Mshambuaji Moses Phiri amepangwa kuongoza safu ya ushambuliaji katika mchezo wetu wa leo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Namungo utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.
Phiri atapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo watatu washambuliaji Pape Sakho, Kibu Denis na Augustine Okrah.
Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin wataendelea kuongoza idara ya kiungo wa ulinzi huku Joash Onyango na Henock Inonga wakisimama kama walinzi wa kati.
Kikosi kamili kilivyopangwa
Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Sadio Kanoute (13), Pape Sakho (10), Mzamiru Yassin (19), Kibu Denis (38), Moses Phiri (25), Augustine Okrah (27).
Wachezaji wa Akiba
Beno Kakolanya (30), Erasto Nyoni (18), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Mohamed Ouattara (33), Victor Akpan (6), Nassor Kapama (35), John Bocco (22), Habibu Kyombo.