Kikosi chetu leo saa 12 jioni kitashuka katika Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa Mkoani Lindi kuikabili Namungo kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.
Kikosi cha Leo kina mabadiliko ya mchezaji mmoja ukilinganisha na kile kilichocheza mechi ya fainali ya Kombe la Muungano dhidi ya Azam FC wikiendi iliyopita.
Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mgunda amemuanzisha Edwin Balua akichukua nafasi ya Saido Ntibazonkiza ambaye ni majeruhi.
Hiki hapa kikosi kamili kilichopangwa:
Ayoub Lakred (40), Israel Patrick (5), Zimbwe Jr (15), Kennedy Juma (26), Che Malone (20), Babacar Sarr (33), Willy Onana (7), Fabrice Ngoma (6), Freddy Michael (18), Kibu Denis (38), Edwin Balua (37).
Wachezaji wa Akiba:
Ally Salim (1), Hussein Abel (30), David Kameta (3), Hussein Kazi (16), Abdallah Hamis (13), Saleh Karabaka (23), Pa Omar Jobe (2)