Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya Namungo

Leo saa 10 jioni kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam kuikabili Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Kaimu Kocha Mkuu, Daniel Cadena amefanya mabadiliko ya wachezaji watatu ukilinganisha na kile kilichocheza mchezo uliopita dhidi ya Yanga.

Cadena amempanga Ayoub Lakred kuchukua nafasi ya Aishi Manula, Mzamiru Yassin amechukua nafasi na Sadio Kanoute wakati Willy Onana akichukua nafasi ya Kibu Denis.

Kikosi Kamili kilivyopangwa:

Ayoub Lakred (40), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Che Malone (20), Henock Inonga (29), Mzamiru Yassin (19), Fabrice Ngoma (6), Clatous Chama (17), Jean Baleke (4), Said Ntibazonkiza (10), Willy Onana (7).

Wachezaji wa Akiba

Aishi Manula (28), David Kameta (3), Hussein Kazi (16), Kennedy Juma (26), Abdallah Hamis (13), Luis Miquissone (11), John Bocco (22), Moses Phiri (25), Shaban Chilunda (27).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER