Mshambuliaji Habib Kyombo amepangwa kuongoza mashambulizi dhidi ya Mlandege katika mchezo wa kwanza wa Michuano ya Kombe la Mapinduzi Visiwani Zanzibar.
Kyombo atapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji Kibu Denis, Nelson Okwa, Michael Joseph na Augustine Okrah.
Nassor Kapama atacheza pamoja na Kennedy Juma kama mabeki wakati huku Jimmyson Mwanuke na Gadiel Michael wakicheza pembeni.
Kikosi Kamili kilivyopangwa
Beno Kakolanya (30), Jimmyson Mwanuke (21), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Nassor Kapama (35), Jonas Mkude (20), Kibu Denis (38), Nelson Okwa (8), Habibu Kyombo (32), Michael Joseph (45), Augustine Okrah (27).
Wachezaji wa Akiba
Ally Salim (1), Maulid Juma (50), Pasco Yasita (54), Omary Mfaume (53), Victor Akpan (6), Hassan Mussa (52), Joseph Mbaga (49), Seif Suleiman (36).
