Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya Mbeya City leo

Nahodha John Bocco ataendelea kuongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa leo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Uwanja wa Sokoine saa 10 jioni.

Katika mchezo uliopita ambao tuliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Ruvu Shooting Bocco aliongoza mashambulizi na kupiga hat trick.

Bocco atasaidiana na kinara Moses Phiri ambapo wapata msaada kutoka kwa viungo wawili washambuliaji Clatous Chama na Augustine Okrah.

Kikosi kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Jonas Mkude (20), Clatous Chama (17), Mzamiru Yassin (19), John Bocco (22), Moses Phiri (25), Augustine Okrah (27).

Wachezaji wa Akiba

Beno Kakolanya (30), Erasto Nyoni (18), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Mohamed Ouattara (33), Victor Akpan (6), Pape Sakho (10), Habibu Kyombo (32), Kibu Denis (38).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER