Mshambuliaji Kibu Denis ataendelea kuongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa leo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.
Kibu atapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji wawili Pape Sakho na Rally Bwalya kama ilivyokuwa katika mchezo uliopita.
Katika eneo la kiungo wa ulinzi kutakuwa na watu watatu Erasto Nyoni, Mzamiru Yassin na Sadio Kanoute.
Mlinda mlango Beno Kakolanya ataendelea kusimama kwenye milingoti mitatu kama katika mchezo wa Mbeya City ambao alionyesha kiwango bora.
Kikosi Kamili kilivyopangwa
Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5), Gadiel Michael (15), Henock Inonga (29), Pascal Wawa (6), Erasto Nyoni (18), Mzamiru Yassin (19), Sadio Kanoute (13), Kibu Denis (38), Rally Bwalya (8), Pape Sakho (10)
Wachezaji wa Akiba
Ally Salim (1), Kennedy Juma (26),
Taddeo Lwanga (4), Yusuf Mhilu (27), Medie Kagere (14), Peter Banda (11), Jimmyson Mwanuke (21).