Nahodha John Bocco ataendelea kuongoza safu ya ushambuliaji katika mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC utakaopigiwa leo saa 10 jioni Uwanja wa CCM Kirumba.
Baada ya kukosekana kwa kinara Moses Phiri leo kocha Juma Mgunda amewapanga viungo watatu washambuliaji kumsaidia Bocco.
Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin kama kawaida wataendelea kuongoza safu ya kiungo wa walinzi huku Joash Onyango na Henock Inonga wakisimama kama walinzi wa kati.
Kikosi Kamili kilivyopangwa
Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Sadio Kanoute (13), Clatous Chama (17), Mzamiru Yassin (19), John Bocco (22), Pape Sakho (10), Augustine Okrah (27).
Wachezaji wa Akiba
Beno Kakolanya (30), Erasto Nyoni (18), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Mohamed Ouattara (33), Victor Akpan (6), Nelson Okwa (8), Habibu Kyombo (32), Kibu (38).