Kama kawaida Kocha Mkuu Juma Mgunda ameendelea kuamini katika washambuliaji wawili baada ya kuwapanga Nahodha John Bocco na Moses Phiri kuongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa leo dhidi ya Kagera Sugar.
Mara zote Mgunda amekuwa muumini ya washambuliaji wawili na baada ya kupona majeraha kwa Nahodha Bocco ameungana na Phiri kuongoza mashambulizi.
Wawili hao watapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji Clatous Chama na Pape Sakho.
Kikosi kamili kilivyopangwa
Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12) Mohamed (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Sadio Kanoute (13), Clatous Chama (17), Mzamiru Yassin (19), John Bocco (22), Moses Phiri (25), Pape Sakho (10).
Wachezaji wa Akiba
Beno Kakolanya (30), Erasto Nyoni (18), Kennedy Juma (26), Mohamed Ouattara (33), Jonas Mkude (20), Victor Akpan (6), Kibu Denis (38), Habibu Kyombo (32), Augustine Okrah (27).