Kikosi chetu leo saa moja usiku kitashuka katika Uwanja wa Azam Complex kuikabili Ihefu FC katika mchezo wa Robo Fainali ya Azam Sports Federation (ASFC).
Kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amefanya mabadiliko mawili ukilinganisha na kikosi kilichocheza mechi iliyopita ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca.
Robertinho amewaanzisha Israel Patrick akichukua nafasi ya Shomari Kapombe na Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ anayechukua nafasi ya Gadiel Michael.
Kikosi kamili kilivyopangwa
Aishi Manula (28), Israel Patrick (5), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Erasto Nyoni (18), Clatous Chama (17), Mzamiru Yassin (19), Jean Baleke (4), Saido Ntibazonkiza (39), Kibu Denis (38).
Wachezaji wa Akiba:
Beno Kakolanya (30), Jimmyson Mwanuke (21), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Jonas Mkude (20), Peter Banda (11), John Bocco (22), Mohamed Mussa (14), Pape Sakho (10).