Kocha Mkuu Charles Lukula amefanya mabadiliko ya wachezaji wanne kwenye kikosi cha leo dhidi ya Green Buffalos ukilinganisha na kile kilichocheza na Determine Girls.
Walinzi Violet Nicholas na Diana Mnali wameanza kwenye kikosi cha leo wakichukua nafasi na Esther Erastus na Silvia Thomas wakati viungo washambuliaji Olaiya Barakat na Philomena Abaka wakichukua nafasi za Vivian Corazone na Asha Djafar.
Nahodha Opa Clement ataendelea kuongoza safu ya ushambuliaji sambamba na Aisha Juma wakipewa msaada wa karibu kutoka kwa Pambani Kuzoya, Philomena na Olaiya.
Kikosi Kamili kilivyopangwa
Gelwa Yonah (21), Fatuma Issa (5), Diana Mnali (15), Daniela Kanyanya (22), Violet Nicholas (26), Joelle Bukuru (18), Pambani Kuzoya (17), Olaiya Barakat (9), Aisha Juma (10), Opa Clement (7), Philomena Abakah (6).
Wachezaji wa Akiba
Zubeda Mohamed (20), Dotto Evarist (11) Wema Maile (3), Koku Ally (19), S’arrive Badiambila (2), Topister Situma (13), Vivian Corazone (4), Amina Hemedi (14) Jackline Albert (16), Asha Djafari (24).