Kocha Juma Mgunda, amewapanga nahodha, John Bocco na Moses Phiri kuongoza mashambulizi katika mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi Geita Gold utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza saa 10 jioni.
Bocco na Phiri wametengeneza muelewano mzuri na imekuwa chachu ya ushindi tunaendelea kupata katika mechi zetu.
Wawili hao watapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji, Clatous Chama na Pape Sakho ambao watashambulia kutokea pembeni.
Kikosi kamili kilivyopangwa
Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Sadio Kanoute (13), Clatous Chama (17), Mzamiru Yassin (19), Bocco (22), Moses Phiri (25), Pape Sakho (10).
Wachezaji wa Akiba
Beno Kakolanya (30), Erasto Nyoni (18), Kennedy Juma (26), Mohamed Ouattara (33), Jonas Mkude (20), Victor Akpan (6), Kibu Denis (38), Habibu Kyombo (32), Augustine Okrah (27).