Nahodha John Bocco na kinara Moses Phiri wamepangwa kuongoza mashambulizi katika mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal UnionĀ utakaopigwa Uwanja wa Mkwakwani saa 10 jioni.
Katika mechi zetu kadhaa zilizopita Kocha Juma Mgunda amekuwa akipanga washambuliaji wawili Bocco na Phiri.
Wawili hao watapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji Clatous Chama na Pape Sakho.
Kikosi Kamili kilivyopangwa
Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Sadio Kanoute (13), Clatous Chama (17), Mzamiru Yassin (19), John Bocco (22), Moses Phiri (25), Pape Sakho (10).
Wachezaji wa Akiba
Beno Kakolanya (30), Erasto Nyoni (18), Kennedy Juma (26), Mohamed Ouattara (33), Victor Akpan (6), Jonas Mkude (20), Habibu Kyombo (32), Augustine Okrah (27), Jimmyson Mwanuke (21).