Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya Coastal Leo

Leo 9:30 Alasiri kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Uhuru kuikabili Coastal Union katika mchezo wa Ligi ya NBC ambao utakuwa wa mwisho katika msimu wa 2022/23.

Kocha Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amefanya mabadiliko ya mchezaji wawili ukilinganisha na kikosi kilichocheza juzi dhidi ya Polisi Tanzania.

Robertinho amewaanzisha Nassor Kapama na John Bocco wakichukua nafasi za Henock Inonga na Jean Baleke.

Kikosi Kamili kilivyopangwa:

Ally Salim (1), Shomari Kapombe (12), Israel Patrick (5), Kennedy Juma (26), Erasto Nyoni (18), Nassor Kapama (35), Peter Banda (11), Jonas Mkude (20), John Bocco (22), Saido Ntibanzonkiza (39), Kibu Denis (38).

Wachezaji wa Akiba

Beno Kakolanya (30), Ahmed Teru (31), Gadiel Michael (2), Mohamed Mussa (14), Jean Baleke (4), Habib Kyombo (32), Jimmyson Mwanuke (21)

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER