Leo saa 10 jioni kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam kuikabili Al Masry katika mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Kocha Fadlu Davids amefanya mabadiliko ya mchezaji mmoja akilinganisha na kile kilichoanza mchezo wa mzunguko wa kwanza kule Suez Canal.
Fadlu amemuanzisha mshambuliaji, Steven Mukwala akichukua nafasi ya, Leonel Ateba ambaye yupo benchi.
Hiki hapa kikosi kamili kilichopangwa:
Moussa Camara (40), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Karaboue Chamou (2), Abdurazak Hamza (14), Yusuph Kagoma (21), Kibu Denis (38), Fabrice Ngoma (6), Steve Mukwala (11), Jean Charles Ahoua (10), Elie Mpanzu (34).
Wachezaji wa Akiba:
Ally Salim (1), David Kameta (3), Valentine Nouma (29), Edwin Balua (37), Ladaki Chasambi (36), Debora Fernandes (17), Awesu Awesu (23), Leonel Ateba (13), Joshua Mutale (26).