Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya Al Dhafrah leo

 

Nahodha John Bocco amepangwa kuongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa kwanza wa kirafiki hapa Dubai dhidi ya Al Dhafrah utakaopigwa mjini Abu Dhabi saa 10 jioni.

Bocco atapata msaada wa karibu kutoka viungo watatu washambuliaji, Clatous Chama, Saido Ntibazonkiza na Pape Sakho.

Katika eneo la katikati ya uwanja Kocha Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amewapanga Jonas Mkude na Sadio Kanoute kwenye kiungo wa ulinzi.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Kennedy Juma (26), Jonas Mkude (20), Pape Sakho (10), Sadio Kanoute (13), John Bocco (22), Said Ntibazonkiza (39), Clatous Chama (17).

Wachezaji wa Akiba

Beno Kakolanya (30), Ally Salim (1), Jimmyson Mwanuke (21), Gadiel Michael (2), Mohamed Ouattara (33), Erasto Nyoni (18), Nassor Kapama (35), Mzamiru Yassin (19), Habibu Kyombo (32), Kibu Denis (38).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER