Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya Al Ahly

Leo saa 12 jioni kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Al Ahly katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya African Football League (AFL).

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amefanya mabadiliko ya wachezaji wawili ukilinganisha na kikosi kilichocheza mechi ya mwisho ya ligi dhidi ya Singida Fountain Gate.

Mlinzi wa kati Henock Inonga amerejea kikosini kuchukua nafasi ya Kennedy Juma huku Luis Miquissone akichukua nafasi ya nahodha, John Bocco.

Kikosi Kamili kilichopangwa

Ally Salim (1), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Che Malone (20), Henock Inonga (29), Fabrice Ngoma (6), Mzamiru Yassin (19), Saido Ntibazonkiza (10), Kibu Denis (38), Clatous Chama (17), Luis Miquissone (11).

Wachezaji wa Akiba:

Ayoub Lakred (36), Israel Patrick (5), David Kameta (3), Kennedy Juma (26), Husseni Kazi (16), Sadio Kanoute (8), Abdallah Hamisi (13), Moses Phiri (25), Willy Onana (7), Jean Baleke (4), Shaban Chilunda (27), John Bocco (22).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER