Kikosi chetu leo saa 10 jioni kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Bravos Do Marquis katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Kocha Fadlu Davids amefanya mabadiliko ya wachezaji wanne ukilinganisha na kikosi kilichocheza mechi ya mwisho ya Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Pamba Jiji.
Kocha Fadlu amewaanzisha Mohamed Hussein, Abdulrazack Hamza, Augustine Okajepha na Kibu Denis kuchukua nafasi za Valentine Nouma, Karaboue Chamou, Debora Fernandes na Awesu Awesu.
Hiki hapa kikosi kamili kilichopangwa:
Moussa Camara (40), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Abdulrazack Hamza (14), Che Malone (20), Fabrice Ngoma (6), Ladaki Chasambi (36), Augustine Okajepha (25), Leonel Ateba (13), Jean Charles Ahoua (10), Kibu Denis (38).
Wachezaji wa Akiba:
Aishi Manula (28), Valentine Nouma (29), Karaboue Chamou (2), Debora Fernandes (17), Mzamiru Yassin (19), Awesu Awesu (23), Joshua Mutale (26), Steven Mukwala (11), Edwin Balua (37)