Kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi saa moja usiku katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Maafande wa Ruvu Shooting.
Kocha Mkuu Robertinho amefanya mabadiliko ya wachezaji wawili ukilinganisha na kile kilichocheza na Azam FC katika mchezo wa nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup.
Robertinho amewaanzisha Jonas Mkude na Kennedy Juma wakichukua nafasi za Sadio Kanoute mwenye kadi nyekundu na Henock Inonga.
Kikosi Kamili kilivyopangwa
Ally Salim (1), Shomari Kapombe, Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Kennedy Juma (26), Jonas Mkude (20), Clatous Chama (17), Mzamiru Yassin (19), Jean Baleke (4), Saido Ntibazonkiza (39), Kibu Denis (38).
Wachezaji wa Akiba
Ahmed Teru (31), Israel Patrick (5), Erasto Nyoni (18), Ismael Sawadogo (3), Pape Sakho (10), Nassor Kapama (35), John Bocco (22), Habibu Kyombo (32), Peter Banda (11).