Kikosi kitakacho tuwakilisha dhidi ya Mbeya Kwanza Leo

Baada ya kukosekana katika mechi mbili kutokana na maumivu ya mguu kiungo mkabaji Sadio Kanoute, amerejea kikosini na leo ameanza dhidi ya Mbeya Kwanza.

Kanoute atacheza sambamba na Jonas Mkude katika eneo la kiungo wa ulinzi kuhakikisha mabeki wetu wanakuwa salama.

Mlinzi wa kati Pascal Wawa ameanza katika kikosi cha leo akichukua nafasi ya Joash Onyango ambaye amepumzishwa.

Kocha Pablo Franco leo ameanza na washambuliaji wawili Medie Kagere na nahodha John Bocco ambao watapata huduma ya karibu kutoka kwa viungo washambuliaji Pape Sakho na Rally Bwalya.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

 Aishi Manula (28), Israel Patrick (5), Mohamed Hussein (15), Henock Inonga (29), Pascal Wawa (6), Jonas Mkude (20), Pape Sakho (10), Sadio Kanoute (13), Medie Kagere (14), John Bocco (22), Rally Bwalya (8).

Wachezaji wa akiba

Beno Kakolanya (30), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Erasto Nyoni (18), Hassan Dilunga (24), Mzamiru Yassin (19), Chris Mugalu (7), Clatous Chama (17), Jimmyson Mwinuke (21).

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER