Kikosi kitakacho tuwakilisha dhidi ya KMC leo

 

Moses Phiri amepangwa kuongoza safu ya ushambuliaji katika mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC utakaopigwa leo Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Phiri ambaye amefunga mabao mawili kwenye mechi zetu mbili za kwanza atapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji Clatous Chama, Pape Sakho na Augustine Okrah.

Nassor Kapama na Sadio Kanoute wamepangwa katika idara ya kiungo waulinzi huku Henock Inonga na Mohamed Ouattara wakiongoza safu ya ulinzi.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Israel Patrick (5),
Mohamed Hussein (15), Henock Inonga (29), Mohamed Ouattara (33), Nassor Kapama (35), Pape Sakho (10), Sadio Kanoute (13), Moses Phiri (25), Clatous Chama (17), Augustine Okrah (27).

Wachezaji wa Akiba

Beno Kakolanya (30), Erasto Nyoni (18), Kennedy Juma (26), Mzamiru Yassin (19), Kibu Denis (38), Nelson Okwa (8), Dejan Georgijevic (7), Habibu Kyombo (32), John Bocco (22).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER