Alfajiri ya kesho kikosi cha Wachezaji 22 benchi la ufundi pamoja na baadhi ya watu kutoka kwenye Menejimeti wataanza safari kuelekea nchini Angola kwa ajili ya mchezo wa tano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Bravos Do Marquis.
Mchezo dhidi ya Bravos utapigwa Jumapili Januari 12 saa moja usiku.
Hiki hapa Kikosi kamili kitakachosafiri:
Makipa:
Moussa Camara, Hussein Abel na Ally Salim
Mabeki:
Karaboue Chamou, Che Malone Fondoh, Abdurazak Hamza, Mohamed Hussein, Shomari Kapombe na Kelvin Kijili.
Viungo:
Mzamiru Yassin, Fabrice Ngoma, Yusuph Kagoma, Elie Mpanzu, Augustine Okejepha, Kibu Denis, Debora Fernandes, Ladaki Chasambi, Awesu Awesu, Edwin Balua na Jean Charles Ahoua
Washambuliaji:
Leonel Ateba na Valentino Mashaka