Kikosi kilichopangwa dhidi ya Dodoma Jiji

Muda mchache ujao kikosi kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Uhuru kuikabili Dodoma Jiji kwenye mchezo wa pili wa Ligi Kuu ya NBC.

Kocha Mkuu, Robertinho amefanya mabadiliko ya wachezaji wawili ukilinganisha na kile kilichoanza dhidi ya Mtibwa Sugar.

Kiungo mkabaji, Mzamiru Yassin ameanza kuchukua nafasi ya Sadio Kanoute na Said Ntibazonkiza akichukua nafasi ya Kibu Denis.

Kikosi kamili kilivyopangwa:

Ally Salim (1), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Che malone Fondoh (20), Kennedy Juma (26), Fabrice Ngoma (6), Mzamiru Yassin (19), Saidi Ntibazonkiza (10), Jean Baleke (4), Essomba Onana (7), Clatous Chama (17)

Wachezaji wa akiba:

Hussein Abeli (30), Israel Mwenda (5), Hussein Kazi (16), Abdallah Hamis (13), Sadio Kanoute (8), Luis Miquissone (11), Denis Kibu (38), John Bocco (22), Moses Phiri (25).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER