Kikosi Kamili kitakachopaa jioni ya Leo kuifuata Al Merreikh

Kocha Mkuu, Didier Gomes Da Rosa ameweka hadharani kikosi cha wachezaji 25 kitakachopaa jioni ya leo kuelekea nchini Sudan kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Merreikh utakaopigwa siku ya Jumamosi.

Katika kikosi hicho yupo pia mlinda mlango namba moja Aishi Manula ambaye alipata majeruhi kwenye mchezo wa Ligi uliopita dhidi ya JKT Tanzania tulioibuka na ushindi wa mabao 3-0 lakini yuko fiti na tayari kwa mtanange.

Nahodha John Bocco ambaye amekosa mechi mbili za mwanzo dhidi ya AS Vita na Al Ahly kutokana na kutokuwa fiti nae yupo kikosini tayari kwa mchezo huo.

Kikosi Kamili Kitakachosafiri

MAKIPA

 1. Aishi Manula
 2. Benno Kakolanya
 3. Ally Salum

WALINZI

 1. Shomari Kapombe
 2. David Kameta
 3. Gadiel Michael
 4. Mohammed Hussein
 5. Joash Onyango
 6. Pascal Wawa
 7. Erasto Nyoni
 8. Kennedy Juma
 9. Peter Muduhwa

VIUNGO

 1. Taddeo Lwanga
 2. Jonas Mkude
 3. Hassan Dilunga
 4. Mzamiru Yassin
 5. Clatous Chama
 6. Luis Miquissone
 7. Rally Bwalya
 8. Ibrahim Ajibu
 9. Francis Kahata

WASHAMBULIAJI

 1. John Bocco
 2. Medie Kagere
 3. Miraji Athumani
 4. Chris Mugalu
SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER