Kikosi Kamili chaondoka kuelekea Morogoro

Kikosi chetu kimeondoka kuelekea mkoani Morogoro tayari kwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa Uwanja wa Jamhuri saa 10 jioni.

Kabla ya kuondoka kikosi kimefanya mazoezi ya mwisho asubuhi katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena tayari kwa mchezo huo.

Tumeondoka na kikosi kamili kuelekea Morogoro ambapo hakuna mchezaji yoyote ambaye amesalia isipokuwa nahodha John Bocco anayeendelea kuuguza majeraha.

Kwa sasa kila mchezo tumeupa umuhimu mkubwa na alama tatu ndio malengo yetu, tunafahamu Prisons ipo kwenye kiwango bora kwa sasa lakini tumejipanga kuwakabili.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER