Kikosi chawasili salama Zanzibar

Kikosi chetu kimewasili salama Visiwani Zanzibar tayari kwa kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Machi 29 Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Tumesafiri na wachezaji wote ambao hawako kwenye majukumu ya timu za Taifa lengo likiwa kuwaweka tayari na mchezo huo mkubwa ambao tunahitaji kupata ushindi.

Baada ya kikosi kufika Zanzibar leo saa tatu usiku kitafanya mazoezi ya utimamu wa mwili kwa ajili ya kuweka miili sawa na kesho kitaendelea na programu ya mazoezi.

Tumechagua kuweka kambi Zanzibar kutokana na utilivu wake huku pia kukiwa na nafasi ya timu kufanya mazoezi usiku.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER