Kikosi chatua salama Tabora kuifuata KMC

Kikosi chetu kimetua salama mkoani Tabora tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC utakaopigwa Ijumaa katika Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi.

Mara ya mwisho kucheza mechi mkoani hapa ilikuwa Aprili 18, mwaka 2017 dhidi ya Rhino Rangers ambapo ulikuwa ni mchezo wa kirafiki na tuliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Afya za wachezaji wetu zinaendelea kuimarika kwa kiasi kikubwa na tumesafiri na karibia kikosi kizima kwa ajili ya kutafuta alama tatu muhimu.

Baada ya kikosi kuwasili wachezaji watapumzika kidogo na jioni watafanya mazoezi ya kuweka miili sawa kuelekea mchezo huo.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER