Kikosi chetu kimewasili salama jijini Dar es Salaam kutoka mkoani Tabora baada ya mchezo wa jana wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC uliopigwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Baada ya kutua Dar es Salaam wachezaji wamepewa mapumziko mafupi kusherehekea Sikukuu ya Christmas pamoja na familia zao.
Baada ya Sikukuu kumalizika kikosi kitarejea mazoezini kujiandaa na mchezo ujao wa ligi dhidi ya Azam FC utakaopigwa Januari Mosi Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.
Jambo jema ni kwamba afya za wachezaji zinaendelea kuimarika siku hadi siku na matarajio yetu hadi kufika siku hiyo kikosi kitakuwa kamili.